Kwa Mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) limetangaza kuwa vikosi vyake vya ulinzi wa anga vimefanikiwa kudungua ndege isiyo na rubani ya Marekani aina ya MQ-9 baada ya kile kilichoelezwa kuwa ni vitendo vya uchokozi na uingiliaji wa kijeshi wa Marekani katika eneo la Ghuba ya Uajemi.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mfumo wa ulinzi wa anga wa IRGC pia uliilazimisha ndege nyingine isiyo na rubani aina ya RQ-4 pamoja na ndege ya kivita ya F-35 kuondoka katika anga ya Iran baada ya kufyatuliwa risasi za moja kwa moja za onyo na ulinzi wa anga.
IRGC imesisitiza kuwa vikosi vyake viko tayari kujibu uvamizi wowote au ukiukwaji wa usitishaji mapigano, na imeonya kuwa hatua yoyote ya uchokozi kutoka Marekani itakabiliwa na majibu ya haraka na ya kulipiza kisasi.
Your Comment